1 Kings 12:22-24

22Lakini neno hili la Mungu likamjia Shemaya mtu wa Mungu: 23“Mwambie Rehoboamu mwana wa Sulemani mfalme wa Yuda, na nyumba yote ya Yuda na Benyamini, na watu wengine wote, 24‘Hili ndilo asemalo Bwana: Msipande kupigana dhidi ya ndugu zenu, Waisraeli. Nendeni nyumbani, kila mmoja wenu, kwa kuwa hili nimelitenda mimi.’ ” Kwa hiyo wakalitii neno la Bwana na kurudi nyumbani, kama Bwana alivyokuwa ameagiza.

Ndama Wa Dhahabu Huko Betheli Na Dani

Copyright information for SwhKC